NAFASI ZA MASOMO MWANGA SEKONDARI
Shule ya sekondari Mwanga inayomilikiwa na Jumuiya ya wazazi Tanzania ya mchanganyiko wavulana na wasichana itoayo elimu kuanzia kidato Cha 1 hadi Cha 6,shule ya Mwanga sekondari ni Kitovu cha elimu Kwa wanafunzi wanatoka familia za kipato cha chini ,mikoa mbalimbali Tanzania
Pichani ni mkuu wa shule ya sekondari Mwanga Bi Mena Kengera.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkuu wa shule Mena Kengera amesema kuwa shule ya Sekondari Mwanga, inapokea wanafunzi wanaotoka katika mazingira mbalimbali na imekuwa ikitoa elimu Bora mwaka hadi mwaka
Shule inapokea wanafunzi wa madhehebu yote na inamlea mwanafunzi kulingana na maadili ya dhehebu lake.
Mwanga Sekondari ina mazingira rafiki ya kujifunzia wanafunzi na ina miundo mbinu ya kisasa, maabara za sayansi zenye vifaaa vya kisasa,madarasa ya kutosha,maktaba yenye vitabu vya kutosha na mandhari nzuri,
Walimu mahiri waliobobea katika masomo mbalimbali yakiwemo masomo ya sayansi, Sanaa biashara. Masomo yanayofundishwa kwa kidato Cha Tano na sita ni katika tahasusi za PCM,PCB CBG, ,EGM,HGE,ECA,HKL,HGL NA HGK.
Mwelekeo wa shule kitaaluma ni mzuri Kwa kuwa kiwango Cha ufaulu katika mitihani ya taifa kuwa juu, ambapo kwa kidato Cha 6 miaka 3 mfulilizo shule ya Mwanga sekondari imeweza kutoa matokeo mazuri yenye mjongeo chanya mwaka hadi mwaka. Kama ifuatavyo:
Mwaka: I II III IV O
2021 11 28 26 - -
2022 10 27 19 - -
2023 20 30 05 01 -
Matokeo ya 2023 yalikuwa mazuri zaidi kwa kuwa idadi kubwa ya wanafunzi walifaulu kwa kiwango cha Division I and II
Shule ya sekondari Mwanga imeendelea kupokea medali na tuzo mbalimbali kutokana na ushiriki wake katika michezo mbalimbali. Mkuu wa shule anatoa rai Kwa wazazi kuwaruhusu watoto kujiunga kwenye michezo mbalimbali kwani michezo ni ajira, pia michezo inachangamsha akili, ikiwemo vijana kuendeleza vipaji vyao.
Mwanga Sekondari inafundisha masomo ya ziada ya ujasiria mali na kompyuta kwa vitendo,hili litasaidia kupunguza ukosefu wa ajira pindi vijana wamalizapo shul
Mkakati wa shule ni kuwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidi ili waweze kupata matokeo bora na kujikwamua kiuchumi.
Shule ya sekondari Mwanga imekuwa na utaratibu wa kila mwaka kutembelea shule rafiki iliyopo nchini Ujerumani ambapo hadi sasa wanafunzi 48 na walimu 11 wamefanikiwa kutembelea shule hiyo rafiki inayoitwa Humboldtschule.
Shule ya sekondari Mwanga inatangaza nafasi za masomo Kwa kidato cha 5 kwa mwaka 2023/2024 na kwa wanafunzi wahamiaji wa kidato Cha 1 na Cha 3 pia shule ya Mwanga Sekondari ni kituo cha watahiniwa wa kujitegema (Private candidates).
Mkuu wa shule anawakaribisha wazazi kuwaleta wanafunzi Mwanga sekondari ili kupata elimu bora kwa gharama nafuu.
Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu Kwa mkuu wa shule ya sekondari Mwanga nambari :0755278551 au namba zifuatazo 0755278551
0712490303
0754 477064
Comments
Post a Comment