KADA YA AFYA NCHINI IMETAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAKE ISIJE KUINGILIWA NA WAGANGA WA KIENYEJI

Na Pendo Mkonyi Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amewataka Wahitimu wa Taasis ya CEDHA Kwenda kuzingatia taaluma yao ipasavyo fani hiyo isije kuingiliwa na waganga wa kienyeji.

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa

Akizungumza katika Mahafali ya 36 ya  taasis ya CEDHA Amewataka Wahitimu kwenda kufanya kazi Kwa weledi na kubadilisha mtazamo wa watu katika kada hiyo ambayo imechafuliwa na watu wachache wasiokuwa waaminifu.

Mtahengerwa amesema kuwa watumishi wa kada hiyo wajitahidi kuwahudumia watu vizuri kwani wasipochangamka  na kutafuta majibu ya  changamoto  zinazoizunguka jamii akina Dr Mwaka watachukua nafasi zenu ilihali hawana elimu ya kuwazidi ninyi.

Zipo changamoto katika kada hiyo yakiwemo malalamiko wakati wa utendaji kazi ambapo wakati mlipokuwa chuoni hamkumfundishwa hivyo lugha za baadihi ya wauguzi zimekuwa chanzo cha wagonjwa wengi  kuzidiwa badala ya kupata tumaini la kupona.

Amesema kuwa mnalo jukumu la kwenda kubadilisha historia Sasa ili kuiponya kada hii haipendezi mtu hajaenda shule aje kukubalika kirahisi na kutoa majawabu na ninyi mpo hapo. 

Kuhitimu kwako kunaenda kuongeza thaman katika maisha yenu 
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anastahili pongezi kufuatia kuboresha mambo mengi katika sekta ya afya kwani zaidi ya billion 6 zimeingia katika jiji la Arusha ili huduma iliyokusudiwa kufika Kwa wananchi ifike Kwa wakati

Pamoja na hayo mkuu wa wilaya hiyo amesema kuwa Kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2023 zaidi ya bilioni 4.5 za kwanza zimetengwa hivyo zipo fedha zitatengwa Kwa ajili ya maboresho ya chuo hicho kufuatia chuo hicho kuwa tegemezi

Kulingana na ulimwengu huu kuwa wa kidigitalni lazima kujiendeleza zaidi na kufanya tafiti ya changamoto  zinazowazunguka haipendezi afrika kuwa sehemu ya kueletewa majawabu ya changamoto zinazotukabili na  badala yake ni Muda wa kubadilika Sasa na kuisaidia jamii na kuendana na Kasi ya teknolojia

Aliwatoa wasiwasi Wahitimu kuhusu chuo chao kuingizwa kwenye  mfumo kwani uwezekano upo endapo  chuo kitakuwa kimekidhi vigezo na mashariti hakuna kizuizi Cha kuingizwa katika mfumo .

Mkuu wa chuo Dr Johannes Lukumay amesema kuwa taasis ya CEDHA ina miaka 40 Sasa tangu ilipoundwa mnamo mwaka 1983 baada ya kilichokuwa chuo Cha Tabibu wasaidizi Kwa kubadilishwa hadhi yake.

Pichani ni mkuu wa taasis ya CEDHA Dr Johannes Lukumay

CEDHA imepewa majukumu manne wakati wa uanzishwaji wake ikiwemo kuwafundisha wakufunzi wa vyuo vya taaluma  za afya,kuwaendeleza kitaaluma watumishi wa sekta ya afya waliopo kazini,kufanya tafiri zenye  kutatua changamoto za sekta ya afya na kutoa ushauri elekezi kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya afya.

Aidha taasis ya CEDHA ina jumla ya watumishi 25  watumishi  wa kada mbalimbali za afya wanaofanya majukumu ya kuendesha  mafunzo na program mbalimbali za taasisi.

Taasis hiyo inatoa mafunzo ya mufupi na muda mrefu kama vile mafunzo ya tiba mpya ya malaria ,mafunzo kuhusu afya ya mama na mtoto,mafunzo ya utawala na uongozi mafunzo ya kuboresha ubora wa huduma za hospital kupitia modo ya FS KAIZEN Mafunzo ya mbinu za kufanya utafaiti,mafunzo ya uandaaji ser na mipango ya huduma za afya katika halmashauri.

Sanjari na hayo  mwaka 2004 wizara iliongeza majukumu taasis na kuifanya kuwa kituo Cha rasilimali Cha Kanda ya kaskazin kikihudumia mikoa minne Manyara,Arusha, Kilimanjaro na Tanga 

Majukumu yaliyoainishwa  ni pamoja na kufanya tafiti juu ya mahitaji ya kitaaluma Kwa watumishi wa afya,kutoa mafunzo ya kuwajengea weledi watumishi wa afya, kutafuta rasilimali za kuwaendeleza kitaaluma watumishi wa afya kuratibu mafunzo yanayotolewa kitaaluma watumishi wa afya.

Taasis ya CEDHA ni pekee tangu kuanzishwa kwake  Kwa kutoa mafunzo ya stashahada ya ualimu wa vyuo vya taaluma za afya nchini Tanzania Baraza na visiwani na jumla ya wakufunzi 617 waliopata mafunzo ngazi ya stashahada waliohitimu na kufanya vizuri wakiwemo wa nchi zingine kama vile Uganda,Kenya, Ethiopia,Sudan ya kusin,Malawi,Namibia  na Botswana.

CEDHA katika uendelezaji wake wa kuisaidia wizara ya afya  imefanya tafiri za afya  zikiwemo zile za ukimwi,afya ya uzazi katika jamii ili kuwaongezea ifahamu zaidi jamii juu ya maswala ya ukimwi na afya ya uzazi, vilevile imeongeza kozi za mafunzo ya Muda mrefu na mfupi katika nyanja ya tiba Kinga,na tafiri za afya.

Katika azma ya kuendeleza kuisaidia wizara na serikali kuboresha huduma katika sekta ya afya , taasis inaendelea kufanya ushirikiano na taasisi,vyuo vikuu,wadau mbalimbali wa kimataifa na WA kitaifa ndani na nje ya inch katika jitihada za kuisaidia serikali,awali ushirikiano kati ya CEDHA na WHO ulilenga juu ya kuimarisha  afya ya msingi katika mikoa yote ya Kanda ya kaskazin.

Taasis ya CEDHA imeendelea kujiendeleza katika kupanua  wigo wa kusaidia  serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia  Suluhu Hassan kwa kubuni na kuanzisha miradi ya afya itqkayonufaishs jamii zetu nchini,kutoa mafunzo ya afya kwenye jamii ngazi ya mtaa,vitongoji, na kata. Ili kuboresha jamii Kwa kujikinga na magonjwa ya mlipuko,magonjwa ya kuambukiza na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanainyemelea jamii.

Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.