CHUO CHA USUSI NA UREMBO EUREKA CHAHITIMISHA WATAALAM 120 SEKTA YA HOTEL NA USUSI KATIKA MAHAFALI YA 14

 Na Pendo Mkonyi Arusha

Wahitimu wapatao 120 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu ngazi ya pili katika fani ya hotelia na ususi  katika  chuo Cha  Eureka Cha jijini Arusha.

Pichani ni Kamishina msaidizi wa mamlaka ya ngorongoro Ramadhani Rashid 

Mara baada ya kuwatunuku vyeti Wahitimu hao Kamishina msaidizi wa mamlaka ya ngorongoro Ramadhani Rashid wakati alipokuwa mgeni rasmi ametoa pongezi Kwa uongozi wa chuo Cha Eureka Kwa kuendelea kupigana vita ya umaskini Kwa kuwasaidia vijana ku kujiajri hata kuajiriwa.

Aliwataka  wazazi na watanzania kufahamu kuwa vyuo hivyo vya kati ni dili sasa kulingana mifumo yake ya kutengeneza ajira kwani vijana wanatoka na ujuzi niseme wazi hii ni fursa hivyo wazazi itumieni vizuri.

Tukio hili muhimu la kuwaaga vijana Kwa kuishi nao vizuri na kuwajengea  uwezo ni somo zuri ili kuwajulisha na wengine kufikia kiwango kama hicho kama Wahitimu waliivyoonesha hapa mbele shughuli zao

Aidha amewaasa Wahitimu kufahamu wao ni mabalozi wa chuo Cha Eureka na katika utendaji kazi kwani utawatengenezea jina na kipato chao na kutangaza chuo  kulingana na huduma nzuri utakayompa mteja ndio itakyokupa fursa ya kuendelea kuwa kwenye soko vinginevyo utafunga biashara Yako kama hauko vizuri.

Eleweni wateja wenu mkiwahudumia vizuri ndivyo watakavyozidi kuwatangaza ninyi wasusi,licha ya kuhitimu hatua fulani bado unayo fursa ya kuendelea kujipanua kielimu na karibu unavyoendelea kuitambulisha kazi Yako japokuwa leo umevaa joho Hilo liwe chachu ya kujiendeleza zaidi ili maisha ya we mazuri

Kulingana na risala iliyowasilishwa na mkuu wa chuo mamlaka itatoa screen tv Kwa ajili ya vijana wazidi kujufunza 

Mkuu wa chuo Cha Eureka frenk Godfrey Kileo amesema kuwa chuo Cha Eureka kilianzishwa mnamo tarehe 5/2/2007 dhamira ikiwa Kila mwanafunzi kupatiwa huduma stahiki na mafunzo mahiri kwa  kuwapa ujuzi Kwa kutengeneza ajira na kupunguza umaskini na shughuli zote za uzalishaji Kwa watanzania
Pichani ni   Mkuu wa chuo Cha Eureka Frenk Godfrey Kileo 

Kupitia chuo Cha Eureka wanafunzi wameweza kupatiwa fani mbalimbali zinazowawezesha  kuwajengea uwezo na kufahamu mafunzo yao ni kitega uchumi kwao na  kwa kuthibitisha hilo zipo fani ambazo hazikuweza kuathiriwa na ugonjwa wa uviko 19 ikiwemo fani ya ususi na ambapo tuanawaona vijana Leo wanahitimu.

Hata hivyo Wahitimu wa chuo Cha Eureka wanawashukuru wazazi na chuo Kwa kuwapa elimu itakayowawezesha kuendesha maisha yao bila ya kipingamizi

Pichani ni afisa masoko Lilian Molel wa chuo Cha Eureka

Afisa masoko Lilian aliwataka wazazi kufahamu kuwa chuo Cha Eureka ni chuo pekee Kanda ya kaskazin Kwa kutoa mafunzo yanayompa kijana kujiajiri ambapo amesekuwa wakufunzi wote wavyuo vya ufundi vya kati vya ususi na urembo wamehitimu Chuo Cha Eureka jijini Arusha.
Amesema chuo Cha Eureka kinakuza vipaji vya vijana pia kinafundisha hata kuandaa filamu kadhalika masuala ya urembo hata kuwapamba maharusi.

Comments

Popular posts from this blog

SHULE YA MCHEPUO WA KIINGEREZA RITALIZA MKOANI KILIMANJARO YATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA MADARA YA AWALI NA MSINGI

MZALIWA WA KWANZA WA NABII MKUU GEOR DAVIE AZIKWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE

CHUO CHA OLOKII CHATANGAZA DIRISHA LA UDAHILI KWA WANAVYUO KWA MWAKA 2023/2024.