KADA YA AFYA NCHINI IMETAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAKE ISIJE KUINGILIWA NA WAGANGA WA KIENYEJI
Na Pendo Mkonyi Arusha Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amewataka Wahitimu wa Taasis ya CEDHA Kwenda kuzingatia taaluma yao ipasavyo fani hiyo isije kuingiliwa na waganga wa kienyeji. Pichani ni mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa Akizungumza katika Mahafali ya 36 ya taasis ya CEDHA Amewataka Wahitimu kwenda kufanya kazi Kwa weledi na kubadilisha mtazamo wa watu katika kada hiyo ambayo imechafuliwa na watu wachache wasiokuwa waaminifu. Mtahengerwa amesema kuwa watumishi wa kada hiyo wajitahidi kuwahudumia watu vizuri kwani wasipochangamka na kutafuta majibu ya changamoto zinazoizunguka jamii akina Dr Mwaka watachukua nafasi zenu ilihali hawana elimu ya kuwazidi ninyi. Zipo changamoto katika kada hiyo yakiwemo malalamiko wakati wa utendaji kazi ambapo wakati mlipokuwa chuoni hamkumfundishwa hivyo lugha za baadihi ya wauguzi zimekuwa chanzo cha wagonjwa wengi kuzidiwa badala ya kupata tumaini la kupona. Amesema kuwa mnalo jukumu la kwenda kubadilisha historia