Posts

DCEA YAPIGA HODI WILAYANI MWANGA; YATOA ELIMU KINGA KWA WANAFUNZI NA JAMII SOKONI MWANGA

Image
Na Prisca Libaga Maelezo, Mwanga Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya Wilaya ya Mwanga tarehe 19.09.2024 imetoa elimu kinga kwa makundi mbalimbali  juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.  Jumla ya watu 2,500 walipatiwa elimu kinga ikihusisha wanafunzi wa Shule za Sekondari za Mwanga, Vudoi na Mandaka pamoja na wafanyabiashara/wachuuzi wa  Soko la Mwanga. DCEA Kanda ya Kaskazini iliwahamasisha wananchi  wa Wilaya ya Mwanga washirikiane na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya waliopo katika maeneo yao wanayoishi kwa kupiga bure namba ya simu 119.

AIRTEL KUBORESHA HUDUMA YA MAWASILIANO YA SIMU NCHINI.

Image
 Na Prisca Libaga Maelezo Arusha  Mkurugenzi wa biashara Kampuni ya simu za mkononi, Airtel ,Joseph Muhere, amesema mwaka Jana kampuni hiyo imefunga mtambo mpya Submarinecable ambao ni mkubwa na una uwezo mkubwa wa kupokea na kutumia data kwa kiwango kikubwa ,uwekezaji huo umefanywa kwa ajili ya Watanzania na nchi jirani ambazo zinahitaji mawasiliano kwa njia ya mtandao. Amesema kuwa kampuni hiyo mwaka huu 2024 inaendelea kufungua huduma  zake za mawasiliano katika miji na Vijiji ambapo kwa mjini watawezesha wateja kupata huduma ya 3G,4G,5G na Kampuni inaendelea na Uwekezaji na upanuzi wa mtandao maeneo ya Vijiji ili kuwezesha kupata huduma ya 3G 4G na 5G Muhere, ameyasema hayo Septemba 18  alipokuwa akizungumza na Vyombo vya habari kwenye kongamano la siku mbili la wadau wa mawasiliano  linalofanyika hoteli ya Gran Melia,Jijini Arusha  Amesema kuwa lengo la Mkutano huo wa 8 ni kuwaleta Wadau wote pamoja katika teknolojia, ambapo kampuni hiyo inaendelea kuvifikia Vijiji vyote ambavyo h

DCEA YAFANYA UTEKETEZAJI WA DAWA ZA KULEVYA AINA YA MIRUNGI JIJINI ARUSHA

Image
Na Prisca Libaga Arusha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa niaba ya Kamishna Jenerali tarehe 13.09.2024 imeteketeza kwa mujibu wa sheria vielelezo vya dawa za kulevya aina ya mirungi kilogramu 23.74 zilizokamatwa katika operesheni zilizotekelezwa hivi karibuni. Uteketezaji wa vielelezo hivyo ulifanyika katika dampo la Murieti jijini Arusha.  Zoezi hilo limeshuhudiwa na wawakilishi kutoka Mahakama ya Wilaya Arusha, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Arusha, Ofisi ya Mkemia Mkuu Arusha kulingana na Matakwa ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. 

TPHPA YAHIMIZA UZALISHAJI WA MAZAO YASIYOTUMIA KEMIKALI ZA SUMU

Image
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Nchini  TPHPA imetilia mkazo wa uzalishaji mazao yasiyo na sumu ili kupanua wigo katika soko la dunia kwa lengo LIKIWA ni kulinda afya za walaji. Na Pendo Mkonyi, Arusha. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa kwanza wa Wadau wa  TPHPA Jijini Arusha, Mkuu wa  Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo Hussein Bashe aliyetarajiwa kuwa Mgeni Rasmi, ameipongeza mamlaka hiyo kwa jitihada zake kubwa za kuleta mabadiliko na uzalishaji wenye tija  katika sekta ya kilimo. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda (katikati kushoto) akipata ufafanuzi wa bidhaa zinazozalishwa na Mamlaka(TPHPA) hiyo kutoka kwa Dkt. Neduvoto Mollel wa kwanza (kulia). Aidha ameongeza kuwa, Sekta ya Kilimo ni mkombozi kwani inategemewa kuongeza ajira kwa jamii hususani vijana na wanawake, kuimarisha mfumo wa chakula na kuongeza pato la taifa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030. "Serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta hii muhimu imeongeza bajeti kutok

KAMPUNI YA UTALII YA KILL FAIR KUKUTANISHA WADAU WA UTALII ZAIDI YA 600 JUNE 7 HADI JUNE 9 JIJINI ARUSHA

Image
Na Pendo Mkonyi,Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii Angela  Kairuki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya Karibu -Kilifair 2024  yanayotarajiwa kufanyika Juni  7 hadi 9 mwaka huu mkoani Arusha . Aidha katika maonyesho hayo wanunuzi zaidi ya 600 wa Utalii kutoka nchi  40 duniani na waonyeshaji pamoja na wadau 468 wa utalii kutoka nchi 37, wamethibitisha kushiriki maonyesho ya kimataifa ya Karibu -Kilifair  yanayotarajia kuanza Juni 7 hadi 9 mwaka huu jijini Arusha. Vile vile wadau hao na wanunuzi  wa  utalii  watatembelea vivutio vya utalii, ili wakawe mabalozi wazuri kwenye nchi zao. Mkurugenzi wa Kili fair Ltd  Dominic Shoo   ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo,amesema lengo la maonyesho hayo ni kutangaza vivutio vilivyopo nchini pamoja na kuonesha tamaduni mbalimbali za kiafrika.  Pichani ni mkurugenzi  wa Kampuni ya Kill fair  Bw Dominic Shoo  Alisema kuwa Kwa takribani siku tatu tunatarajia kuwa na kiwango kikubwa cha biashra kwa sababu leng

“TUSIKATE MITI HOVYO”-DKT. MPANGO

Image
Na Prisca Libaga,Tanga Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Phillip Mpango amewataka wananchi kutokata miti hovyo ili kulinda mazingira na uoto wa asili uliopo sasa. Pichani ni Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango Dkt. Mpango ameyasema hayo leo Februari 21,2024 katika kijiji cha Kabuku wilayani Handeni ikiwa ni siku ya kwanza ya Ziara yake ya Siku tatu mkoani Tanga. Mhe. Dkt. Mpango amewataka wananchi kupanda miti kwa wingi ili kuhifadhi mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabia Nchi ambayo kwa sasa yamepelekea kuwa na joto kali hasa kwa ukanda wa Pwani. Vilevile, Mhe. Dkt Mpango alisisitiza jukumu la kutunza uoto wa asili ni la kila mtanzania hivyo ni vema kushiriki katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti kwa wingi. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) Awali akitolea ufafanuzi wa baadhi ya changamoto zilizotolewa na Mbunge wa Handeni Mjini Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) alimhakikishia Makamu wa Rais k

SERIKALI KUIMARISHA ULINZI WA MALI NA MAISHA YA WATU DHIDI YA WANYAMAPORI WAKALI NA WAHARIBIFU.

Image
Na. Anangisye Mwateba-Dodoma Serikali kupitia Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuimarisha ulinzi wa mali na maisha ya watu dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo yenye changamoto nchini ikiwemo Kiwangwa, Bwilingu, Mkangena na maeneo yanayozunguka Hifadhi ya Pori la Akiba Wami-Mbiki. Pichani ni Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula Haya yamebainika wakati Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula akijibu swali la Mhe. Subira Khamis Mgalu(Mb) aliyetaka kujua Je, Serikali imefikia wapi kuzuia Tembo kuharibu mazao na kuwadhuru wananchi wa Kiwangwa, Bwilingu, Mkange na wanaozungukwa na Hifadhi ya Wami-Mbiki. Mhe. Kitandula alisema  Wizara imechukua hatua ya  Kuweka kambi za muda za Askari na kuwapatia vitendea kazi (magari na pikipiki) kwa ajili ya doria za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu. Mhe. Kitandula aliongeza kuwa hatua nyingine ni kufanya doria za udhibiti wa wanyamapori kwenye maeneo yenye changamoto