Posts

Showing posts from September, 2024

DCEA YAPIGA HODI WILAYANI MWANGA; YATOA ELIMU KINGA KWA WANAFUNZI NA JAMII SOKONI MWANGA

Image
Na Prisca Libaga Maelezo, Mwanga Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya Wilaya ya Mwanga tarehe 19.09.2024 imetoa elimu kinga kwa makundi mbalimbali  juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.  Jumla ya watu 2,500 walipatiwa elimu kinga ikihusisha wanafunzi wa Shule za Sekondari za Mwanga, Vudoi na Mandaka pamoja na wafanyabiashara/wachuuzi wa  Soko la Mwanga. DCEA Kanda ya Kaskazini iliwahamasisha wananchi  wa Wilaya ya Mwanga washirikiane na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya waliopo katika maeneo yao wanayoishi kwa kupiga bure namba ya simu 119.

AIRTEL KUBORESHA HUDUMA YA MAWASILIANO YA SIMU NCHINI.

Image
 Na Prisca Libaga Maelezo Arusha  Mkurugenzi wa biashara Kampuni ya simu za mkononi, Airtel ,Joseph Muhere, amesema mwaka Jana kampuni hiyo imefunga mtambo mpya Submarinecable ambao ni mkubwa na una uwezo mkubwa wa kupokea na kutumia data kwa kiwango kikubwa ,uwekezaji huo umefanywa kwa ajili ya Watanzania na nchi jirani ambazo zinahitaji mawasiliano kwa njia ya mtandao. Amesema kuwa kampuni hiyo mwaka huu 2024 inaendelea kufungua huduma  zake za mawasiliano katika miji na Vijiji ambapo kwa mjini watawezesha wateja kupata huduma ya 3G,4G,5G na Kampuni inaendelea na Uwekezaji na upanuzi wa mtandao maeneo ya Vijiji ili kuwezesha kupata huduma ya 3G 4G na 5G Muhere, ameyasema hayo Septemba 18  alipokuwa akizungumza na Vyombo vya habari kwenye kongamano la siku mbili la wadau wa mawasiliano  linalofanyika hoteli ya Gran Melia,Jijini Arusha  Amesema kuwa lengo la Mkutano huo wa 8 ni kuwaleta Wadau wote pamoja katika teknolojia, ambapo kampuni hiyo inaendelea kuvifikia Vijiji vyote ambavyo h

DCEA YAFANYA UTEKETEZAJI WA DAWA ZA KULEVYA AINA YA MIRUNGI JIJINI ARUSHA

Image
Na Prisca Libaga Arusha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa niaba ya Kamishna Jenerali tarehe 13.09.2024 imeteketeza kwa mujibu wa sheria vielelezo vya dawa za kulevya aina ya mirungi kilogramu 23.74 zilizokamatwa katika operesheni zilizotekelezwa hivi karibuni. Uteketezaji wa vielelezo hivyo ulifanyika katika dampo la Murieti jijini Arusha.  Zoezi hilo limeshuhudiwa na wawakilishi kutoka Mahakama ya Wilaya Arusha, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Arusha, Ofisi ya Mkemia Mkuu Arusha kulingana na Matakwa ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.