TPHPA YAHIMIZA UZALISHAJI WA MAZAO YASIYOTUMIA KEMIKALI ZA SUMU
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Nchini TPHPA imetilia mkazo wa uzalishaji mazao yasiyo na sumu ili kupanua wigo katika soko la dunia kwa lengo LIKIWA ni kulinda afya za walaji. Na Pendo Mkonyi, Arusha. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa kwanza wa Wadau wa TPHPA Jijini Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda aliyemwakilisha Waziri wa Kilimo Hussein Bashe aliyetarajiwa kuwa Mgeni Rasmi, ameipongeza mamlaka hiyo kwa jitihada zake kubwa za kuleta mabadiliko na uzalishaji wenye tija katika sekta ya kilimo. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda (katikati kushoto) akipata ufafanuzi wa bidhaa zinazozalishwa na Mamlaka(TPHPA) hiyo kutoka kwa Dkt. Neduvoto Mollel wa kwanza (kulia). Aidha ameongeza kuwa, Sekta ya Kilimo ni mkombozi kwani inategemewa kuongeza ajira kwa jamii hususani vijana na wanawake, kuimarisha mfumo wa chakula na kuongeza pato la taifa kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030. "Serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta hii muhimu imeongeza bajeti kutok