KAMPUNI YA UTALII YA KILL FAIR KUKUTANISHA WADAU WA UTALII ZAIDI YA 600 JUNE 7 HADI JUNE 9 JIJINI ARUSHA
Na Pendo Mkonyi,Arusha. Waziri wa Maliasili na Utalii Angela Kairuki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya Karibu -Kilifair 2024 yanayotarajiwa kufanyika Juni 7 hadi 9 mwaka huu mkoani Arusha . Aidha katika maonyesho hayo wanunuzi zaidi ya 600 wa Utalii kutoka nchi 40 duniani na waonyeshaji pamoja na wadau 468 wa utalii kutoka nchi 37, wamethibitisha kushiriki maonyesho ya kimataifa ya Karibu -Kilifair yanayotarajia kuanza Juni 7 hadi 9 mwaka huu jijini Arusha. Vile vile wadau hao na wanunuzi wa utalii watatembelea vivutio vya utalii, ili wakawe mabalozi wazuri kwenye nchi zao. Mkurugenzi wa Kili fair Ltd Dominic Shoo ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo,amesema lengo la maonyesho hayo ni kutangaza vivutio vilivyopo nchini pamoja na kuonesha tamaduni mbalimbali za kiafrika. Pichani ni mkurugenzi wa Kampuni ya Kill fair Bw Dominic Shoo Alisema kuwa Kwa takribani siku tatu tunatarajia kuwa na kiwango kikubwa cha biashra kwa sababu leng