“TUSIKATE MITI HOVYO”-DKT. MPANGO
Na Prisca Libaga,Tanga Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Phillip Mpango amewataka wananchi kutokata miti hovyo ili kulinda mazingira na uoto wa asili uliopo sasa. Pichani ni Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango Dkt. Mpango ameyasema hayo leo Februari 21,2024 katika kijiji cha Kabuku wilayani Handeni ikiwa ni siku ya kwanza ya Ziara yake ya Siku tatu mkoani Tanga. Mhe. Dkt. Mpango amewataka wananchi kupanda miti kwa wingi ili kuhifadhi mazingira na kupambana na mabadiliko ya tabia Nchi ambayo kwa sasa yamepelekea kuwa na joto kali hasa kwa ukanda wa Pwani. Vilevile, Mhe. Dkt Mpango alisisitiza jukumu la kutunza uoto wa asili ni la kila mtanzania hivyo ni vema kushiriki katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti kwa wingi. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) Awali akitolea ufafanuzi wa baadhi ya changamoto zilizotolewa na Mbunge wa Handeni Mjini Mhe. Kwagilwa Reuben Nhamanilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) alimhakikishia Makamu wa Rais k